Maelekezo Ya Awali Uzinduzi wa TIMS

HOME 18/11/2020

Kwa wanachama wote

TUCASA STU itazindua mfumo wa TIMS Rasmi Tarehe 20/11/2020

NAMNA ya kuupata mfumo, utaingia kwenye tovuti rasmi ya TUCASA STU (www.tucasastu.com) Utaenda kwenye Menu kisha utaona kwa chini sehemu imeandikwa TIMS utabonyeza Na itakupeleka moja Kwa moja kwenye MFUMO.

TIMS NI NINI
TIMS ni kifupi cha neno TUCASA INFORMATION MANAGEMENT SYSTEM
Huu ni mfumo wa kimtandao unaohusisha udhibiti na utunzaji wa taarifa za TUCASA. Ni mfumo utakao muwezesha mwanachama kuona taarifa mbalimbali na maendeleo ya chama kiganjani mwake, ikiwepo taarifa za malipo yake binafsi pamoja na maendeleo ya kiroho tawini kwake

NAMNA YA KUJISAJIRI MWENYEWE KWENYE MFUMO WA TIMS(TUCASA INFORMATION MANAGEMENT SYSTEM)

1. Namna ya kujisajiri
Kwenye ukurasa wa kuingia utaona maneno yameandikwa Register here Bonyeza hapo kisha itatokea fomu ya kujisajiri yenye hatua nne 4 fuata MAELEKEZO kwa kila kisanduku ambapo utahitajika kuweka maelezo yako binafsi kama
Majina yako yote
Hapa weka majina yako sahihi yanayotambulika tawini kwako au chuoni

Namba yako ya simu weka namba inayopatikana (weka namba yako sahihi kwani ndiyo itakayotumika wakati wa kuthibitisha(approve) akaunti yako, kwani hakuna akaunti itakayothibitishwa kama ina namba ambayo si sahihi na pia utatambuliwa kwa namba hiyo wakati wote kutakapotokea changamoto kwenye system )

Weka email address yako iweke kwa usahihi maana itatumika wakat wa kurekebisha (ku-reset) password yako ikipotea au kusahaulika

Weka jinsia yako
Chagua Me kama mwanaume Na Ke kama mwanamke

Baadae bofya kitufe kilichoandikwa next Utaenda hatua ya pili ambapo utaweka maelezo yafuatayo

Maelezo ya ubatizo
Chagua Yes kama umebatizwa Na No kama bado hujabatizwa

Password
Weka password yenye tarakimu au namba zisizopungua nane ambazo utazikumbuka kirahisi (N.B utakapoweka chini ya hizo hautaweza kuruhusiwa kuingia kwenye mfumo hata kama umekuwa approved )

Start year
Chagua mwaka wako wa kuanza masomo Na kama mwaka wako hauonekani mtaarifu kiongozi wako atakusaidia.

End year
Chagua mwaka unaotegemea kumaliza Chuo kama ulivyosajiliwa Na Chuo husika

Baadae bofya kitufe kilichoandikwa next Utaenda hatua ya tatu ambapo utaweka maelezo yafuatayo

Course name
Weka Course unayosoma chuoni kwa kirefu mfano: Bachelor of Science in Chemistry

Select your university
Kwenye Sanduku(box) hili andika Chuo unachosoma kwa kirefu au ufupisho(Abbreviation) utaona Chuo chako, aidha kama hautaona Chuo chako mtafute kiongozi yeyote wa TUCASA au tuma Ujumbe kwenda 0756770473 utasaidiwa kwa haraka.

Select Member Position
Hapa chagua nafasi yako, kama ni mwanachama wa kawaida chagua Member, kama ni kiongozi chagua Nafasi(position) yako. Ikiwa nafasi(position) fulani ya uongozi haionekani, Mtafute kiongozi wa TUCASA wa ngazi ya juu yako au piga simu/Ujumbe kwenda 0756770473 utasaidiwa.
Kumbuka kuchagua chaguo sahihi ili anayekuidhinisha aweze kukutambua kirahisi, tofauti na hivyo akaunti yako haitaidhinishwa.

Place of resident
Andika sehemu/Mtaa unaoishi kama ni ndani ya Chuo andika jina la Hostel Na namba ya chumba chako mfano: Hostel Block no 6A, Room 245

Baadae bofya kitufe kilichoandikwa next Utaenda hatua ya nne Na ya mwisho ambapo utaweka maelezo yafuatayo:-

Select Your Zone
Chagua kanda yako unaweza ukaandika kwenye kisanduku itakuja kwa urahisi, kisha ibofye.

Select Your Conference
Chagua Jimbo lako unaweza ukaandika kwenye kisanduku, itakuja kirahisi, kisha ibofye.

Baada ya hapo bofya register utaletewa maneno ya blue-bahari yaliyoandikwa
“Congrats you have Been registered please wait for approval”
Hapo itakubidi usubiri mpaka kiongozi wa tawi lako atakapohakiki na kujiridhisha na taarifa zako.
Kama itachukua mda mrefu akaunti yako haijahakikiwa muone katibu wa tawi lako husika atakusaidia kuidhinisha kwa wakati

NB: kama akaunti yako haijahakikiwa utakapojaribu kuingia itakuambia Incorrect username or password hii ni kwasababu taarifa zako bado haijahakikiwa na kuidhishwa na katibu wako wa tawi

Imetolewa Na Idala ya Mawasiliano TUCASA STU
18 Nov. 2020
Kwa mawasiliano
Barua Pepe info@tucasastu.com
Contact: 0756770473, 0679528022