MWALIKO WA KUHUDHURIA MKUTANO MKUU WA CHAMA UTAKAOFANYIKA KATIKA MUCE IRINGA

HOME 02/04/2021

Nawasalimu katika Jina la Yesu Kristo.
Husika na kichwa cha barua tajwa hapo juu. Uongozi wa TUCASA Jimbo Kuu kwa niaba ya
viongozi wengine wote unawapongeza sana wanachama wote waliojitoa kuhudhuria mkutano
wetu mkuu wa chama, zaidi tunamshukuru MUNGU kwasababu ya wema na baraka zake toka
tulipoachana mwaka jana mwezi Machi pale Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu MKWAWA.
Uongozi unawakaribisha sana katika mkutano mzuri ulioandaliwa vizuri katika mazingira mazuri
sana ya Mkoa wa Iringa. Imani yetu ni kuwa tutakuwa na wakati mzuri sana wa kukutana kama
marafiki na kufurahi pamoja na zaidi kukutana na Mungu wetu. Tutajifunza, tutaimba, na tutapata
wakati wa kuburudika, kwa michezo na programu mbalimbali. Tunapojiandaa kwa ajili ya
kuhudhuria mkutanoni tunapenda kutoa taarifa juu ya mambo yafuatayo:

1. HALI YA HEWA
Hali ya hewa ya Iringa ni ya ubaridi na kuna mvua zinanyesha mara kwa mara. Hivyo tunashauriwa
kufika na mavazi ambayo yatatusitiri kama vile sweta, jaketi na shuka nzito za kujifunika.

2. AFYA
Tunaomba radhi kwa kutohusisha gharama za bima ya Maisha kwenye kiingilio, hivyo tunaomba
Mungu atulinde tusafiri na kurudi salama. Kuhusu swala la matibabu kila mmoja afike na bima
yake ya matibabu kwa wale walionazo. Ikiwa mwanachama hana bima hiyo basi afike na gharama
za tahadhari kwa ajili ya matibabu. Vilevile kila mwanachama achukue mahitaji yake muhimu
kama vile mswaki, dawa ya meno na sabuni.

3. MUSIC CONCERT
Tunapenda kuwaalika wanachama wote katika sherehe ya ufunguzi wa mkutano itakayoambatana
na uimbaji. Kwaya mbalimbali kutoka Iringa zimekwishaalikwa na hivyo tusikubali kupitwa na
mibaraka hiyo tuwahi kuwasili mkutanoni. Tamasha hilo litaanza saa 8:00 mchana hadi saa 1:00
jioni.

4. COMMUNITY IMPACT
Tutakuwa na tukio la kufikia jamii wakati wa mkutano wetu. Kulingana na ratiba yetu siku ya
ijumaa mbali na matembezi katika vivutio mbalimbali vya utalii tutafikia jamii kwa huduma
mbalimbali. Miongoni mwa huduma hizo ni kutembelea vituo vya watoto yatima na utoaji wa
damu.

5. NAMBA ZA USAJILI
Tunapenda kuwasisitiza wanachama kuhakikisha kuwa kila mmoja anayo namba ya usajili
inayotolewa katika orodha ya majina kwa kila jimbo. Ikiwa mwanachama haoni jina lake na alitoa
kiingilio awasiliane na wahazini mapema.

PETER N KANUDA
KATIBU MKUU TUCASA STU