Summit ni neno la kingereza lenye maana ya mkutano wa kilele. Mkutano huu unafanyika mwishoni mwa mwaka ambapo kwa taifa la israel ulifuatia baada ya sikukuu ya upatanisho, na baada ya mavuno.
Baada ya kutafakari juu ya sikukuu hii ya kilele iliyofanywa na Israel kila mwisho wa mwaka nashawishika kushiriki nawe mambo kadhaa juu ya sikukuu hii ambayo ni muhimu kwetu pia kama wa Israel wa Kiroho “… Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli” Warumi 9:6.
Nini maana ya Sikukuu ya vibanda(SUMMIT ya Israel)
“Sikukuu ya Vibanda haikuwa tu ya ukumbusho bali ilikuwa ya kipekee. Haikuashiria tu kukaa jangwani, lakini, kama sikukuu ya mavuno, iliadhimisha ukusanyaji wa matunda ya dunia, na kuelekeza mbele kwa siku kuu ya ukusanyaji wa mwisho, wakati Bwana wa mavuno atakapotuma wavunaji kukusanya magugu pamoja katika mafungu kwa moto, na kukusanya ngano katika ghala Lake”. Wazee&Manabii 541.2
Kwanini nasi tunapaswa kushiriki SUMMIT kama ilivyokuwa kwa Israel?
“Wakati wana wa Israeli walisherehekea ukombozi ambao Mungu alikuwa amewafanyia baba zao, na kuwahifadhi kwake kimiujiza wakati wa safari zao kutoka Misri, ndivyo tunapaswa kukumbuka kwa shukrani njia anuwai ambazo Bwana amebuni kututoa ulimwenguni, na kutoka giza la upotovu, kuingia katika nuru ya thamani ya neema yake na kweli. Wazee na manabii” 540.6
Kwa upande wa wanafunzi walioko vyuoni, baada ya kupata mavuno katika Elimu, Uchumi, mahusiano yao nk, mwishoni mwa mwaka wao wa kiutendaji(mwaka wa TUCASA), Huu ni muda kwa wao kwenda kumshukuru Bwana kwa wema na fadhiri zake kwa siku saba.
Hasara za kutohudhuria SUMMIT
“Pamoja na wale ambao waliishi mbali na maskani, zaidi ya mwezi wa kila mwaka lazima ulitumika katika kuhudhuria karamu za kila mwaka. Mfano huu wa kujitolea kwa Mungu unapaswa kusisitiza umuhimu wa ibada ya kidini na umuhimu wa kutiisha masilahi yetu ya ubinafsi, ya kidunia chini ya yale ya kiroho na ya milele. Tunadumisha hasara tunapopuuza fursa ya kuungana pamoja kuimarishana na kutiana moyo katika utumishi wa Mungu. Ukweli wa neno lake(Mungu) hupoteza uwazi na umuhimu wake katika akili zetu. Mioyo yetu huacha kuangazwa na kuamshwa na ushawishi wa kutakasa, na tunapungua katika hali ya kiroho. Katika tendo letu kama Wakristo tunapoteza mengi kwa kukosa kuoneana huruma”.
Bwana anapoandaa mikutano ya kiroho analo kusudi kubwa kwa maisha yetu. Ni hasara kubwa sana kukosa moja ya baraka hizi. Baada ya kazi Bwana anahitaji upumzike miguuni pake kwa walau siku 7 kwa mwaka.
kuna hatari gani kwa asiye jumuika akibaki kujifunza mwenyewe?
Yeye anayejifunga mwenyewe hajazishi nafasi ambayo Mungu ameipanga anayopaswa kuifikia. Sisi sote ni watoto wa Baba mmoja, tunategemeana kwa furaha. Madai ya Mungu na ya ubinadamu yapo juu yetu. Ni kilimo sahihi cha vitu vya kijamii vya asili yetu ambavyo hutuleta katika huruma na ndugu zetu na hutupatia furaha katika juhudi zetu za kuwabariki wengine”. Wazee&Manabii 541.1
Tunapata furaha katika kujumuika, naam! mtunga zaburi anasema, “Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza,
Ndugu wakae pamoja, kwa umoja” Zaburi 133:1.
Nakusihi jenga tabia ya kuhudhuria mikutano ya kiroho inayoandaliwa bila kujali gharama “Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona” 2Wakorintho 5:7. Bwana mmiliki wa vyote atakujazi. Amini ukatii.
Hesabu faida zaidi ya gharama na dhamiria moyoni mwako kutokosa makambi/mikutano yoyote inapoandaliwa.
Usisite kushiriki(share) na mwingine baraka hizi.
Behold! He is coming