TAARIFA YA MAKABIDHIANO SEC

HOME 01/05/2021

Awali ya yote tunamshukuru MUNGU wa mbinguni kwa wema na upendo wake kwetu, tangu tulipo kabiziwa kijiti cha kutumika shambani mwake hadi sasa tunapoenda kukabizi. Ni hakika amekuwa Pamoja nasi katika kila hatua hatukuona mahali alipo tupungukia Jina lake litukuzwe sana.
Tunawashukuru walezi wetu Pr. Samweli Michael, Pr.Isack Panga, Pr. Mwakalindile na Pr. Gibson kwa jinsi walivyo kuwa bega kwa bega Pamoja nasi, bila kusita kutuelekeza, kutushauri, kututia moyo, kutuombea na kutuonya kwa mengi pale tulipo kosea
MUNGU wa mbinguni awabariki sana.
Shukurani pia kwa viongozi wote wa TUCASA STU, TUCASA SEC, Viongozi wa kanda zote CODAZO, SODAZO, SOZO Bila kusahau viongozi wa matawi, Kwa jinsi tulivyo shirikiana kufanikisha utume tuliopewa kama jimbo kwa mwaka wa uongozi 2020/2021.
Mwisho tunawashuuru wanachama wote na washiriki wa makanisa lezi, kwa jinsi tulivyo shikamana kwa Pamoja, mwenyezi MUNGU awabariki sana.

Taarifa hii ya utendaji kazi jimbo la kusini mashariki mwa Tanzania, imeandaliwa na uongozi wa TUCASA Jimbo la SEC 2020/2021